Polisi Uturuki yawakamatwa waandamanaji kadhaa Mei Mosi
1 Mei 2026
Vyama vya ndani vya wafanyakazi pamoja na Chama cha Wanasheria wa Maendeleo (CHD), kimeliarifu shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba idadi ya waliozuiliwa ilikuwa zaidi ya 350.
Kulingana na mwakilishi mmoja wa CHD, waandamanaji kadhaa tayari wamefikishwa katika makao makuu ya polisi, huku baadhi wakiripoti kupata majeraha walipokuwa wakipelekwa kizuizini. Hata hivyo idadi kamili ya waliozuiliwa haikuweza kuthibitishwa mara moja.
Nchini Ujerumani, wafanyakazi waliandamana kote nchini humo huku vyama vya wafanyakazi vikilalamika kuhusu mipango ya kupunguza huduma za afya na faida ya usalama wa kijamii.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Ujerumani DGB Yasmin Fahimi, amewaambia maelfu ya waandamanaji waliojitokeza kwamba ikiwa watashambuliwa watajilinda na kwamba lazima wabaki kuwa tayari kwa malumbano katika wiki ama miezi ijayo.