1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi 15 nchini Kenya wameshtakiwa kuivamia familia moja

Daniel Gakuba
22 Januari 2021

Maafisa 15 wa polisi ya Kenya wameshtakiwa kuivamia familia moja, na kuwafyatulia watu wake mabomu ya kutoa machozi wakiwa nyumbani kwao na kuwapiga, katika operesheni ya kuzuia maambukizi ya COVID-19.

https://p.dw.com/p/3oHG4
Kenia Nairobi Coronavirus Ausgangssperre Patrouille Kontrolle
Picha: Getty Images/AFP/Y. Chiba

Polisi hao na maafisa wengine sita wa uongozi wa kaunti wanashutumiwa kuivamia familia hiyo katika eneo la Busia magharibi mwa Kenya, mnamo siku za mwanzo za kupambana na virusi vya corona mwezi Machi mwaka jana.

Bodi ya kushughulikia uwajibikaji wa polisi nchini Kenya, IPOA imesema vitendo hivyo viliiumiza vibaya familia ya mwenye nyumba, Bernard Orenga, mkewe na watoto wao, pamoja na majirani zao.

Watuhumiwa hao watasimamishwa kizimbani katika mji wa Bungoma Februari mosi. Juni mwaka jana, afisa mwingine wa polisi ya Kenya alifunguliwa mashtaka ya mauaji ya mtoto wa miaka 13, aliyepigwa risasi akiwa kwenye baraza la nyumba yao, katika operesheni ya polisi kuwataka watu wasitoke majumbani.