PESHAWAR : Shambulio kwa madrasa lauwa watu 80 | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

PESHAWAR : Shambulio kwa madrasa lauwa watu 80

Jeshi la Pakistan limesema limeuwa takriban watuhumiwa waasi 80 katika shambulio kwenye shule ya mafunzo ya dini ya Kiislam au madrasa kaskazini mwa nchi hiyo.

Madrasa hiyo ilioko karibu na mpaka na Afghanistan ilikuwa inaendeshwa na kiongozi wa Taliban katika eneo hilo ambaye alikuwa akitafutwa na serikali kwa kuwapa hifadhi wanamgambo.Haikuweza kujulikana iwapo alikuwa miongoni mwa watu waliopoteza maisha yao.Msemaji wa jeshi amesema operesheni hiyo ilihusisha vikosi vya majeshi na helikopta za mashambulizi na kwamba ilikuwa inazingatia sera ya serikali ya Pakistan ya kutokomeza ugaidi.

Shambulio hilo limelaaniwa nchini kote Pakistan na waandamanaji katika eneo hilo wanadai kwamba wote waliouwawa walikuwa ni raia wa kawaida.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com