1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

PEGIDA

PEGIDA – Wazalendo wa Ulaya dhidi ya kuenezwa kwa Uisilamu katika mataifa ya Magahribi – ni vuguvugu lililoanzia mjini Dresden, Ujerumani, ambalo limekuwa likiitisha maandamano ya umma tangu Oktoba 2014.

Kundi hilo linalojiita “Patriotische Europäer gegen die Islamisierung des Abendlandes” liliasisiwa na Lutz Bachmann na kuvutia uungwaji mkono kutoka sehemu mbalimbali za nchi, ambapo raia waliingia mitaani katika maandamano ya ndani yanayoandaliwa na matawi ya PEGIDA. Lilikosolewa na kuchochea maandamano ya kulipinga, ambayo mara nyingi yalikuwa yanayapiku ya kwake. Wanasiasa nchini Ujerumani, wakiwemo Rais Joachim Gauck na Kansela Angela Merkel, walitahadharisha kwamba maandamano ya PEGIDA yanawakilisha chuki dhidi ya wageni na ubaguzi wa rangi.