1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi ya Ujerumani yajiweka tayari kwa maandamano Chemnitz

Sekione Kitojo
30 Agosti 2018

Polisi ya Ujerumani inajiweka tayari kwa maandamano ya watu wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia leo(30.08.2018)dhidi ya sera za  uhamiaji za kansela  Angela Merkel katika mji wa mashariki mwa Ujerumani wa Chemnitz.

https://p.dw.com/p/343eP
Deutschland Demonstration der rechten Szene in Chemnitz
Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Meyer

Hali  hiyo  imezuka kutokana  na  shambulio  la  kuchomwa  kisu mtu  mmoja  na  kufariki limezusha ghasia  za  makundi ya  kibaguzi. Polisi  ya  jimbo  la  Saxony imesema itapata  msaada  wa  polisi  zaidi  kutoka  majimbo mengine  matano  pamoja  na  polisi  kutoka  serikali kuu ya  shirikisho, baada  ya  kuzidiwa  idadi  kwa  kiasi kikubwa  na  maelfu  ya  wanazi, mamboleo, wahuni katika  michezo na  watu  wengine  wenye  misimamo mikali  katika  ghasia  za  siku  ya  Jumapili  na Jumatatu.

Kabinetts-Pressekonferenz mit Michael Kretschmer
Waziri mkuu wa jimbo la Saxsony Michael Kretschmer kutoka chama cha CDUPicha: picture-alliance/dpa/M. Skolimowska

Mji wenye  matatizo  wa  Chemnitz , ambako  waziri  mkuu wa  jimbo  hilo  Michael  Kretschmer  alikuwa  afanye mkutano utakaojadili  demokrasi, umeshuhudia  kuzuka kwa  ghasia zilizokuwa  zikitokota  kwa  muda  mrefu kutokana  na   ghadhabu zilizosababishwa  na  kile waandamanaji  wanachosema  kuwa  ni "uhalifu  wa wahamiaji" tangu  pale  alipouwawa  mtu  mmoja  kwa kuchomwa  kisu  siku  ya  Jumapili.

Polisi  wamewakamata  Yousif Ibrahim A, kutoka  Iraq mwenye umri  wa  miaka  22,  na  Alaa S. kutoka  Syria mwenye  umri  wa  miaka  23, kwa  kumchoma  kisu  Daniel H.  fundi seremala mwenye  umri  wa  miaka  35, uhalifu ambao  ulizusha  mashambulizi  mitaani  dhidi  ya  watu ambao  magenge  hayo  yaliwaona  kuwa  ni  wageni.

Deutschland Demonstration der rechten Szene in Chemnitz
Waandamanaji wa mrengo mkali wa kulia wakiandamana mjini ChemnitzPicha: Imago/Michael Trammer

Matukio  hayo  ya  kuchukiza, ambayo  yalishuhudia mashambulizi  dhidi  ya  mtu  mmoja  kutoka  Afghanistan, Syria  na  Bulgaria  na yamezusha  hali  ya  mabadiliko  ya mawazo  ndani  na  nje  ya  Ujerumani.

Ashambuliwa kwa minyororo ya chuma

Katika  uhalifu  mwingine uliosababishwa  na  chuki  usiku  katika  eneo  la  mashariki  la  iliyokuwa  Ujerumani  ya kikomunist , mhamiaji  mwenye  umri  wa  miaka  20 alishambuliwa  kwa  matusi  ya  chuki  dhidi  ya  wageni, alipigwa mateke  na  kupigwa  na  minyororo  wa  chuma na watu  watatu  katika  mji  wa  pwani  ya  habari  ya  baltic wa  Wismar, polisi  imesema  bila  kueleza  anatoka  nchi gani.

Chemnitz - Proteste der Rechten mit Plakat mit blutigen Frauengesichtern
Maandamano mengine ya kupinga wenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia mjini ChemnitzPicha: picture-alliance/AP Photo/J. Meyer

Picha  za  waandamanaji  wakitoa salaam iliyopigwa marufuku  ya  enzi  za  utawala  wa  Hitler  katika maandamano  ya  siku  ya  Jumatatu , zilikuwa  zinashitua, "  alisema  mkuu  wa  haki  za  binadmu  wa  Umoja  wa mataifa  Zeid Ra'ad Al-Hussein , akiwataka  wanasiasa kutoka  mataifa  yote  ya  Ulaya  kukemea  hali  hiyo.

Kansela  Angela Merkel ambaye  yuko  katika  ziara  ya mataifa  ya  Afrika  hadi  Ijumaa, kwa  kiasi  kikubwa kujadili  jinsi  ya  kupambana  na  sababu  za  uhamiaji kwenda  Ulaya, ameshutumu maandamano  hayo  ya wenye  msimamo  mkali  wa  mrengo  wa  kulia, akisema hakuna  nafasi  kwa "chuki katika  mitaa"  katika  taifa  hilo la  demokrasia ya  kiliberali.

Karte Deutschland Dresden Chemnitz Berlin EN
Ramani ya jimbo la Saxsony

Uhalifu unaofanywa  na  wahamiaji  mara  nyingi huchukuliwa  na  waungaji  mkono  wa  chama  cha mrengo  mkali  wa  kulia  cha  Alternative  for  Germany, chama  mbadala  kwa  Ujerumani AfD, pamoja  na vuguvugu  la  maandamano  ya  mitaani  la Wazalendo  wa Ulaya  wanaopinga  Uislamu, PEGIDA , ambao wanamuona  Merkel  kama  msaliti kwa  kuruhusu wahamiaji  kuingia  nchini  humo.

Mwandishi: Sekione  Kitojo/afpe

Mhariri: Mohamed Khelef