Papa Leo XIV asafiri kuelekea Guinea ya Ikweta
21 Aprili 2026
Matangazo
Siku ya Jumatatu akiwa nchini Angola, Papa Leo alilaani vitendo vya rushwa na unyonyaji unaofanywa na wenye nguvu dhidi ya wanyonge, na kwamba matumaini ya wengi yanakatishwa tamaa na ghasia zinazotumiwa ili kuwanufaisha matajiri.
Kiongozi huyo wa kiroho ametoa wito wa usambazaji wa haki wa rasilimali za Afrika akisema kuwa ukosefu wa haki unaharibu mioyo, huku mali za wengi zikimilikiwa na wachache.