1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKimataifa

Papa Leo atoa rai ya kusitishwa mapigano siku ya Krismasi

24 Desemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV ametoa mwito wa kusitishwa mapigano kwenye mizozo yote duniani wakati wa sikukuu ya Krismasi kesho Alhamisi.

https://p.dw.com/p/55ugb
Papa Leo XIV
Papa Leo XIV.Picha: Maria Grazia Picciarella/SOPA Images/IMAGO

Akizungumza akiwa kwenye makaazi yake ya mapumziko nje kidogo ya mji wa Roma, Baba Mtakatifu Leo amesema anarejea ombi lake kwa watu wote wenye nia njema kuifanya Krismasi kuwa siku ya amani, kwa angalau kuonesha heshima kwa siku hiyo ya kuzaliwa Yesu Kristo.

Papa Leo pia ameelezea masikikito yake makubwa kwamba Urusi imekataa kuweka chini silaha kwenye vita vinavyoendelea nchini Ukraine hata wakati wa Krismasi.

Wakristo duniani watasherehekea sikukuu ya Krismasi hapo kesho kukumbuka kuzaliwa kwa Yesu zaidi miaka 2000 iliyopita.