Papa Leo ahimiza amani akiwa kwenye ziara yake Algeria
15 Aprili 2026
Kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV ametembelea chimbuko lake la kiimani katika eneo la kale alikozaliwa Mtakatifu Augustine katika mji wa Annaba, nchini Algeria.
Papa Leo alivutiwa kujiunga na upadri kutokana na utumishi wa mwanatheolojia huyo aliyeacha taathira katika ulimwengu wa Ukristo.
Ameliambia kundi dogo la watawa na wazee katika mji huo wa Annaba, kwamba moyo wa Mungu umenyong'onyezwa na vita, vurugu, ukosefu wa haki na uwongo.
Papa Leo XIV kufanya ziara mjini Annaba nchini Algeria
Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa kiroho wa Kanisa Katoliki duniani nchini Algeria, ambako Papa Leo analenga kusisitiza kuhusu ujumbe wa amani pamoja na mshikamano kati ya Wakristo na Waislamu, akitumia muongozo wa Mtakatifu Augustine.
Ziara hiyo ya Papa imekumbwa na mashambulizi mawili ya kujitowa muhanga yaliyotokea katika mji wa Blinda, ulioko kilomita 45 kutoka mji mkuu, Algiers. Kesho Jumatano ataanza ziara yake nchini Cameroon.