1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis ahitimisha ziara Msumbiji

Amina Mjahid
6 Septemba 2019

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis akikamilisha ziara yake nchini Msumbiji, amewasihi viongozi wa kisiasa na kiuchumi wa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mali ghafi wasikubali kuhongwa na watu kutoka nje.

https://p.dw.com/p/3PAQb
Mosambik Papst Besuch Zimpeto
Picha: Reuters/Y. Nardi

Papa Francis ameitembelea hospitali wanakoshughulikiwa watu walioambukizwa virusi vya Ukimwi, na kuongoza misa mbele ya watu 60 elfu katika uwanja wa michezo wa mjini Maputo.

Katika vituo vyote hivyo viwili, Papa Francis alitilia mkazo mada nne muhimu katika ziara yake hii ambazo ni amani, kupambana na umaskini, rushwa na ulinzi wa mazingira.

Baada ya Msumbiji, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amepangiwa kuvitembelea pia visiwa vya Madagascar na Mauritius.

Vyanzo: dpa,reuters