1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Ombi la Oscar Pistorius kuondoka jela mapema lakataliwa

31 Machi 2023

Ombi la msamaha la bingwa wa zamani wa michezo ya Olimpiki kwa walemavu raia wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, aliyefungwa jela mwaka 2016 kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp limekataliwa

https://p.dw.com/p/4PZAW
Südafrika Pretoria | Oscar Pistorius vor Gericht
Picha: Alon Skuy/AP/picture alliance

Haya ni kulingana na mamlaka za magereza Afrika Kusini na wakili wa familia ya Steenkamp.

Pistorius alikuwa anakubaliwa kisheria kuwasilisha ombi la msamaha na kuachiwa mapema kutoka jela baada ya kuhudumu nusu ya kifungo chake, jambo alilofanya, ingawa familia ya Steenkamp ilikua inalipinga ombi hilo.

Südafrika Johannesburg | Reeva Steenkamp und Oscar Pistorius
Pistorious alimuuwa mchumbake Reeva SteenkampPicha: Lucky Nxumalo/AFP

Soma pia: Afisa wa magereza ataka Pistorius apewe kifungo cha nyumbani

Na sasa wakili wa familia hiyo, Tania Koen ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba amepokea simu kutoka katika bodi ya msamaha na kuthibitishiwa taarifa hiyo ingawa amesema bodi hiyo itakutana tena baada ya mwaka mmoja kujadili iwapo inaweza kumsamehe Pistorius. 

Idara ya magereza imesema bodi ya msamaha imekuta kuwa Pistorius hajamaliza muda wa chini wa kuwa kifungo unaohitajika ili aachiliwe huru.

Kikao cha kusikiliza ombi hilo la msamaha kilifanyika leo katika jela moja ya viunga vya mji mkuu Pretoria ambako mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 36 anazuiliwa.

Soma pia: Pistorius apatikana na hatia ya mauaji

Wazazi wa Steenkamp, ambao wanapinga kuwachiliwa kwake mapema, wakisema kuwa hawaamini kama mwanariadha huyo wa zamani alisema ukweli kuhusu kilichotokea na hajaonyesha huruma na kujutia kitendo chake, wameukaribisha uamuzi huo.

afp, reuters