1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pistorius apatikana na hatia ya mauaji

3 Desemba 2015

Oscar Pistorius mwanariadha mwenye ulemavu amehukumiwa kwa kosa la mauaji na mahakama kuu ya rufaa Afrika kusini, ambayo imetupilia mbali hukumu ya awali kwa makosa madogo ya kumpiga risasi mpenzi wake mwaka 2013

https://p.dw.com/p/1HGI7
Oscar Pistorius
Picha: picture-alliance/AP Photo

Pistorius sasa atarejeshwa jela baada ya kuachiliwa huru kwa msamaha Oktoba mwaka huu baada ya kutumikia kifungo cha miaka mitano kwa kosa la kuua bila kukusudia. Jaji Eric Leach ameiambia mahakama hiyo kwamba, amemhukumu Pistorius kuwa na hatia ya mauaji, kwa kuwa mtuhumiwa alifanya uhalifu huo kwa nia kamili ya dhati.

Suala hilo ameongeza jaji huyo kwamba litarejeshwa katika mahakama ili kuangalia hukumu sahihi atakayopewa Pistorius.

Amekuwa akitumikia kifungo cha nyumbani baada ya kukaa mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Awali, ilikuwa imeripotiwa kimakosa kwamba rufaa hiyo ilikuwa imetupwa na angeendelea kutumia kifungo cha kuua bila kukusudia.

Pistorius mwenye umri wa miaka 29, mwanariadha anayekimbia kwa miguu ya bandia alimpiga risasi na kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp , majira ya alfajiri siku ya wapendanao miaka miwili iliyopita.

Mwandishi: Bruce Amani/AP
Mhariri: Yusuf Saumu