1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUrusi

Nyota wa mpira wa kikapu Marekani Griner aachiwa na Urusi

8 Desemba 2022

Urusi leo imemuachia huru mchezaji nyota wa mpira wa kikapu kwa wanawake raia wa Marekani Brittney Griner.

https://p.dw.com/p/4KgLK
Russland Moskau SOMMER 2022 | Verhaftung Brittney Griner, US-Basketballspielerin
Picha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Maafisa wa Urusi na Marekani wamesema Brittney Griner ameachiwa katika hatua ya ngazi ya juu ya ubadilishanaji wa wafungwa, huku Marekani ikimuachia Viktor Bout, raia wa Urusi anayejihusisha na uuzaji silaha kimagendo.

Ubadilishanaji huo wa wafungwa umefanyika huko Abu Dhabi na umefanyika wakati wa mivutano mikubwa iliyoko kati ya Marekani na Urusi kuhusiana na vita vya Ukraine.

Makubaliano haya ya kubadilishana wafungwa ambayo ni ya pili kufanyika katika kipindi cha miezi 8 kati ya nchi hizi mbili, yamepelekea kuachiwa kwa mtu maarufu zaidi raia wa Marekani aliyekuwa amefungwa nje ya nchi yake.

Griner ni bingwa mara mbili wa Olimpiki na timu ya taifa ya wanawake ya Marekani.

Rais Joe Biden alizungumza na Griner kwa njia ya simu hapo jana mbele ya mkewe Cherelle, katika ikulu ya White House.