Nigeria: Kundi la Niger Delta kushambulia sekta ya mafuta | Matukio ya Afrika | DW | 17.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Nigeria: Kundi la Niger Delta kushambulia sekta ya mafuta

Kundi hilo limesema mashambulizi hayo yatakuwa ni mabaya zaidi kuwahi kutokea

Kundi la Nigeria la wapiganaji wa Niger Delta Avengers limesema leo kuwa litaanzisha mashambulizi dhidi ya sekta ya mafuta nchini humo katika siku chache zijazo.

Katika taarifa yake iliyoiweka kwenye tovuti kundi hilo limesema mashambulizi hayo yatakuwa ni mabaya zaidi kuwahi kutokea na yatalenga operesheni za mataifa kadhaa katika eneo la bahari kubwa.

Mnamo mwezi Novemba kundi hilo ambalo limeshambulia vituo kadhaa vya mafuta mwaka 2016 lilisema kuwa limesimamisha makubaliano ya kusitisha mapigano.