1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK:Usalama waimarishwa mjini New York

7 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEU9

Maafisa mjini New York Marekani wamesema wameongeza usalama katika mfumo wa usafiri katika eneo hilo.

Hii inakuja baada ya polisi kupokea taarifa za kitisho dhidi ya usalama katika mji huo.

Kamishna wa polisi mjini New York Ray Kelly amewaambia waandishi wa habari kwamba wasafiri huenda wakatarajia kuongezeka kwa polisi katika mfumo wa usafiri katika kipindi cha siku kadhaa zijazo.

Akizungumza kwenye mkutano huo na wanahabari Mayor wa mji wa New York Michael Bloomberg amesema tahadhari hiyo imetolewa na idara ya upelelezi wa masuala ya jinai.

FBI siku kadhaa zilizopita lakini taarifa hizo hazikutolewa hadharani mara moja kutokana na sababu za kiutekelezaji.