NEW YORK: Eritrea iondoshe vikosi vyake mpakani | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NEW YORK: Eritrea iondoshe vikosi vyake mpakani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon ametoa mwito kwa Eritrea kuondosha majeshi yake kutoka eneo la mpaka wake na Ethiopia ambako vikosi hivyo vinazuiliwa.Kwa mujibu wa ripoti ya Ban iliyotolewa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,Eritrea tangu mwezi wa Septemba imeimarisha vikosi vyake katika eneo la mpakani.Wachambuzi wanaonya kuwa kuna hatari ya kuripuka mapigano mapya.

Kati ya mwaka 1998 na 2000,watu 70,000 waliuawa katika vita vya mpakani kati ya majirani hao wawili kwenye Pembe ya Afrika.Vita hivyo pia vimesababisha maafa makubwa katika nchi ambazo ni miongoni mwa madola masikini kabisa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com