1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu atarajia kuingia awamu ya pili ya makubaliano

7 Desemba 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema leo kwamba anatazamia kuingia katika awamu ya pili ya mpango wa kusitisha mapigano Gaza unaofadhiliwa na Marekani "hivi karibuni".

https://p.dw.com/p/54uIR
Israel Jerusalem 2025 | Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Marekani mjini Jerusalem, Februari 16, 2025Picha: Ohad Zwigenberg/AFP

Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari baada ya mkutano na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz , Netanyahu amesema walijadili jinsi ya kukomesha utawala wa Hamas katika Ukanda wa Gaza na kwamba wamemaliza sehemu ya kwanza.

Pia amesema baada ya muda mfupi wanatarajia kuingia katika awamu ya pili, ambayo ni ngumu zaidi.

Netanyahu amesema atakutana na Rais Donald Trump baadaye mwezi huu, akisema awamu ya pili ya mpango huo wa amani wa Marekani iko karibu.

Waziri huyo Mkuu wa Israel pia amesema kuwa mwishoni mwa mwezi, atakuwa na mazungumzo muhimu sana ya jinsi ya kuhakikisha awamu hiyo ya pili inapata ufanisi.