Nawaz Shariff arejea nyumbani Pakistan | Habari za Ulimwengu | DW | 25.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nawaz Shariff arejea nyumbani Pakistan

Islamabad:

Polisi nchini Pakistan wameanzisha opereshini ya kamata kamata katika wakati huu ambapo waziri mkuu wa zamani Nawaz Shariff anasubiriwa kurejea nyumbani.Msemaji wa chama cha chama cha Nawaz Shariff-Muslim League, amesema mamia ya wafuasi wao wametiwa mbaroni.Polisi wamezinfunga njia zinazotokea Lahore kuelekea uwanja wa ndege.Hata hivyo wafuasi wa Nawaz Shariff wamesema hawatakubali kutishwa.Mamia wamekusanyika katika mji wa Lahore kumlahiki kiongozi huyo wa upande wa upinzani,anaetazamiwa kurejea leo mchana kutoka uhamishoni Saud Arabia .Waziri mkuu huyo wa zamani ambae serikali yake ilitumiliwa madarakani na Pervez Muasharaff mnamo mwaka 1999,anapanga kupigania kiti uchaguzi mkuu utakapoitishwa january nane ijayo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com