Nawaz Sharif arejea Pakistan . | Habari za Ulimwengu | DW | 26.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Nawaz Sharif arejea Pakistan .

Islamabad. Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan Nawaz Sharif amejaza karatasi za kuteuliwa kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu januari siku moja baada ya kurejea nchini humo kutoka uhamishoni nchini Saudi Arabia. Lakini mwanasheria mkuu wa serikali ya Pakistan anariporiwa kusema kuwa Sharif huenda akazuiwa kushiriki katika uchaguzi huo mkuu kutokana na hukumu yake ya kifungo cha maisha kabla ya kwenda kuishi uhamishoni mwaka 2000. Sharif amesema baada ya kuwasili kuwa amerejea na atashiriki katika uchaguzi.

Sharif na ujumbe wake walizingirwa na wafuasi wake jana Jumapili baada ya ndege iliyomchukua kutua mjini Lahore. Jaribio la kwanza la waziri mkuu huyo wa zamani kurejea nchini humo kutoka uhamishoni alikokuwa akiishi kwa muda wa miaka saba lilishindwa miezi miwili iliyopita wakati rais Pervez Musharaf alipoamuru kurejeshwa uhamishoni saa chache baada ya kurejea.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com