1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nani atamfunga paka kengele katika Bundesliga

Sekione Kitojo
18 Septemba 2020

Bayern Munich inaanza leo (18.09.2020)kusaka taji lake la tisa la Bundesliga, na iwapo kuna timu inaweza kuwavua ubingwa, washukiwa wa kawaida wametajwa, wakiongozwa na Borussia  Dortmund.

https://p.dw.com/p/3ifZA
DW Bundesliga Radio Live - Spieltag 1 (HAU)

Hata mwenyekiti wa  Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge  amekiri  kuwa ubabe wao wa kunyakua  mataji manane mfululizo  katika  Bundesliga sio mzuri kwa shauku ya mvuto katika ligi lakini mwishoni mwa siku ni jukumu  la  wapinzani hatimaye kufanya  kitu na  kuwavua taji hilo.

Borussia  Dortmund , klabu ya mwisho  kabla  ya hatua hii  ya  Bayern  kunyakua mfululizo mataji  hayo mwaka  2012, ilikuwa  na  nafasi ya pekee miaka  miwili  iliyopita wakati walikuwa  wakiongoza  kwa  pointi 9 mwezi  Desemba, lakini waliporomoka na kumaliza wakiwa  pointi  mbili  nyuma  ya  mabingwa  hao.

Fußball Borussia Dortmund | Erling Haaland
Erling Haaland wa Borussia DortmundPicha: picture-alliance/SvenSimon/E. Kremser

Mwaka jana RB Leipzig  iliongoza  hadi nusu  ya  kwanza ya msimu lakini  Bayern  ilirejea kutoka kuwa  nyuma  kwa  pointi  saba  muda  mfupi  kabla ya  kuingia  mapumzikoni ya majira  ya  baridi na  kutoroka  tena  na  taji  hilo kwa  kuongoza kwa pointi 13 mbele  ya  timu iliyoshika  nafasi  ya  pili Borussia  Dortmund.

Dortmund, Leipzig, Bayer Leverkusen  na  Borussia Moenchengladbach ni  washukiwa  wa kawaida  linapokuja suala  la  klabu  ambayo  inaweza  kuwapa  changamoto Bayern Munich, na  pia  wametajwa  kuwa  mahasimu  wakuu na  Rummenigge.

Lakini  inaonekana  kuwa juhudi za ziada za kibinadamu zinahitajika  kuwaangusha mabingwa  hao walionyakua  mataji  matatu msimu  huu.

Mshindi asiyeshindika Bayern 

Bayern  hawajafungwa  katika  michezo 20 ya  ligi, ambamo  wameshinda  michezo 19, tangu pale  waliposhindwa  kupata  ushindi  dhidi  ya Leverkusen  na  Gladbach mwishoni  mwa mwezi Novemba  na  mapema  Disemba. Mchezo pekee  waliopoteza  pointi  ni  katika  sare ya  bila  kufungana dhidi ya  RB Leipzig mwezi  Februari.

Kocha  wa  Gladbach Marco Rose wamefurahishwa kusikia  kuwa ni timu inayoweza kuivua ubingwa Bayern lakini  wataweza  kuweka changamoto ya kweli  iwapo watabakia bila ya majeruhi katika  kikosi  chake.

Fußball Bundesliga | Freundschaftsspiel Union Berlin - 1. FC Nürnberg | Mit Fans
Mashabiki kiasi pia wataruhusiwa kushuhudia Bundesliga kwa mara ya kwanza baada ya kuzuka virusi vya coronaPicha: Reuters/H. Hanschke

Iwapo kila  mtu atakuwa katika  afya njema,sisi ni wazuri  sana. "Iwapo kila  mtu atakuwa na hali nzuri ya kiafya, naweza  kuona kikosi chetu katika  nafasi  ya  kushinda dhidi  ya  timu yoyote  katika  ligi," Rose aliwaambia  waandishi  habari siku  ya  Alhamis. Kwa mtazamo huu  ni habari  mbaya  kwamba  Breel Embolo , Valentino Lazaro , Laszlo Benes  na Denis Zakaria ni  majeruhi, kama Rose  alivyosema: Iwapo  wachezaji hao wanne watakuwa  nje kwa  muda  mrefu , ubingwa  huenda  hautakuwapo.

Kwanza  kabisa  kutokuwapo wachezaji  hao kunaweza  kuathiri mchezo  wao  muhimu wa ufunguzi wa  ligi  siku  ya  Jumamosi  dhidi  ya  Dortmund ambao kwa  upande wao wanachukua  tahadhari  kiasi  kuliko  miezi 12  iliyopita na  hawajasema  rasmi wanawania ubingwa.

Kama ilivyo  Gladbach , Dortmund imeweza  kubakisha  kikosi  chao, ambapo ni  Achraf Hakimi  tu  ndie  aliyeondoka  kutoka  katika  kikosi  hicho baada  ya  kumalizika muda wa kuazimwa kutoka  Real Madrid.

Ushambuliaji BvB bado uko shule

Dortmund kwa kiasi  kikubwa itawategemea  vijana  ikiwa  ni  pamoja  na  Jadon Sancho, Erling Haaland, Giovanni Reyna, Jesus Reinier , Jude Bellingham  na  Youssoufa Moukoko ambaye ataweza  tu kucheza  katika  kikosi  cha  kwanza atakapofikisha  umri  wa  miaka  16 katika  majira  ya  mapukutiko mwaka  huu mnamo  mwezi  Novemba.

Deutschland | Fußball Bundesliga Borussia Dortmund Training Youssoufa Moukoko
Yousoufa Moukoko akifanya mazowezi na kikosi cha kwanza cha BvBPicha: AFP/I. Fassbender

Lakini kocha ambaye ni mwenye kuchukua  tahadhari  sana  Lucien Favre ameonya kwamba "katika  ushambuliaji bado tuko shule" wakati  aliomba uvumilivu lakini Dortmund inaonekana kuwa  timu bora  ambayo  inaweza  kuivua  ubingwa  Bayern.

Leverkusen  na  RB Leipzig  ambazo  hazijawahi  kushinda taji  la  Bundesliga, zinakabiliwa na  hali  ya  sintofahamu  baada  ya  kupoteza  wachezaji bora.

Leipzig  ambayo imefikia  nusu  fainali  ya  Champions League imeshuhudia  mfungaji wake bora Timo Werner akitimkia Chelsea  na inaonekana  iwapo Hwang Hee Chan na  huenda pia  Mnorway  Alexander Sorloth wanaweza  kujaza  hilo  pengo.

Fußball | DFB Pokal | FC Nürnberg - RB Leipzig
Mkorea kusini Hee-chan Hwang ambaye anavaa viatu vya Timo Werner katika ushambuliaji katika kikosi cha RB LeipzigPicha: picture-alliance/dpa/D. Karmann

Nahodha  Marcel Sabitzer alisema "Haitakuwa  rahisi hivyo kushinda  ubingwa"  na  kocha mwenye  dhamira Julian Nagelsmann pia  ameeleza kwa tahadhari kuhusu  hilo.

"Unaweza  kuwa  na matundu  katika  utekelezaji  wakati  unashughulika na  kikosi cha vijana. Baadhi  ya  pointi zitapotea  na  itakuwa  vigumu  kufika  juu," Nagelsmann  alisema.