NAIROBI: Washukiwa sita wauwawa kwa kupigwa risasi | Habari za Ulimwengu | DW | 28.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI: Washukiwa sita wauwawa kwa kupigwa risasi

Polisi nchini Kenya wamesema watu sita walioshukiwa kuwa majambazi waliuwawa kwa kupigwa risasi wakati maafisa wa polisi walipokabiliana nao mjini Nairobi Kenya.

Mtoto wa umri wa miaka 10, mwanamume mmoja mzee, maafisa wawili wa polisi na washukiwa wawili walikufa katika mapambano hayo ya risasi.

Mapambano hayo yaliyotokea baada ya maafisa watatu wa polisi kuwatia mbaroni watu wawili walioshukiwa kuwa majambazi wakati walipokuwa wakishika doria kwenye mtaa wa mabanda wa Kariobangi kaskazini mashariki mwa jiji la Nairobi.

Kamanda wa polisi wa eneo hilo, Paul Ruto, amesema hakuna aliyekamatwa katika kisa hicho na hawezi kuthibitisha ikiwa washukiwa hao ni wanachama wa kundi la Mungiki ambalo limekuwa likiwahangaisha Wakenya katika siku chache zilizopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com