Nairobi: Padri akamatwa Kenya kwa madai ya ulawiti | Matukio ya Afrika | DW | 17.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Nairobi: Padri akamatwa Kenya kwa madai ya ulawiti

Polisi nchini Kenya imeripoti kumkamata padri mmoja anaeshutumiwa kufanya mapenzi na mwanaume mwenzake

Polisi nchini Kenya imeripoti kumkamata padri mmoja anaeshutumiwa kufanya mapenzi na mwanaume mwenzake. Polisi imesema jana kwamba wanakijiji wa kaunti ya Muranga katikati mwa Kenya wamekuwa wakimfuatilia padri huyo ambaye wamekuwa wakimshuku kuwa ni shoga na kuvijuulisha vyombo husika baada ya kumuona kijana wa miaka 18 akiingia nyumbani mwa padri huyo Jumatatu iliyopita.

Polisi imesema iliwakuta watu hao wawili wakiwa wamelala juu ya kitanda cha padri na baada ya kuhojiwa wote wawili walikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja.

Mahusiano ya jinsia moja ni kinyume na sheria katika mataifa mengi ya Afrika. Mashoga katika mataifa mengi wanakabiliwa na vitisho, na adhabu ya mahakama.

Sheria ya Kenya inapiga marufuku kitendo cha aina hiyo. Jirani yake Uganda ilipitisha sheria ya kifungo cha maisha kwa baadhi ya vitendo vya ushoga lakini mahakama ya katiba ya nchi ililipinga hilo.