Naibu mkuu wa polisi akamatwa kwa njama dhidi ya waziri mkuu Ethiopia | Matukio ya Afrika | DW | 25.06.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Naibu mkuu wa polisi akamatwa kwa njama dhidi ya waziri mkuu Ethiopia

Idadi ya waliokufa kutokana na shambulizi la guruneti kwenye mkutano wa hadhara katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, imefikia watu wawili.

Watu 30 wamekamatwa kuhusiana na mlipuko huo wakiwemo polisi kadhaa, akiwemo naibu kamishna wa polisi wa Addis Ababa.

Shambulizi hilo lilitokea katika uwanja mkubwa wa wazi uliokuwa umefurika, wakati Waziri Mkuu Abiy Ahmed akikamilisha hotuba yake mbele ya maelfu ya watu siku ya Jumamosi.

Vurugu zilizozuka baada ya mripuko huo wakati watu walianza kukimbilia jukwaani ziliwajeruhi watu 150.

Hakuna aliyetangaza kuhusika na shambulizi hilo lisilo la kawaida katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ambao kila mara huwa na ulinzi mkali.

Ethiopia imesema kuwa Marekani itawatuma wapelelezi wa FBI ili kusaidia kuchunguza shambulizi hilo.

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com