1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Libya yamuachia mwanawe Gaddafi kutoka jela

6 Septemba 2021

Serikali ya Libya imemuachilia huru mtoto wa kiongozi wa zamani wa taifa hilo Moammer Gaddafi, baada ya kufungwa kwa miaka mingi.

https://p.dw.com/p/3zyBQ
Al Saadi Gaddafi Sohn von Muammar Gaddafi Porträt
Picha: Reuters

Saad Gaddafi ameachiliwa huru miaka miwili baada ya uamuzi wa kuachiwa kwake kutolewa. Taarifa kutoka kwa serikali inasema Saad aliachiwa na kupelekwa moja kwa moja kwa familia yake.

Serikali imesema imemuachilia huru kama sehemu ya mpango wa kuwaachia wale waliokamatwa kinyume cha sheria. Saad alikimbilia nchi jirani ya Niger baada ya maandamano ya kutaka mageuzi kuanza mwaka 2011.

Babake  Moammer Gaddafi alikamatwa na kuuwawa na waasi mwezi Oktoba mwaka uo huo. Mwaka 2014 Niger ilimrejesha Saad nyumbani alikofungwa hadi kuachiwa kwake.

Libya imekumbwa na mgogoro tangu kuondolewa na kuuwawa kwa Gadaffi na imekuwa uwanja wa mapambano kwa makundi hasimu ya waasi.