1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Mwanamke wa Uingereza aliejiunga na IS apoteza kesi ya uraia

23 Februari 2023

Mwanamke Muingereza Shamima Begum aliekwenda Syria wakati alipokuwa msichana na kujiunga na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, ameshindwa katika kesi ya rufaa aliyokata ili kupinga kupokonywa uraia wake wa Uingereza

https://p.dw.com/p/4NspA
Shamima Begum
Picha: empics/picture alliance

Serikali ya Uingereza ilimpokonya uraia Shamima Begum kwa misingi ya usalama wa taifa mwaka 2019, muda mfupi baada ya kupatikana katika kambi moja nchini Syria.

Uamuzi huo unamaanisha kuwa Shamima Begum, mwenye umri wa miaka 23, hawezi kurejea Uingereza kutoka katika makazi yake ya sasa katika kambi ya wakimbizi kaskazini mwa Syria.  Anadai kwamba alikuwa muhanga wa "usafirishaji haramu wa watoto" wakati alipojiunga na kundi hilo.

Begum alikuwa na umri wa miaka 15 alipoondoka nyumbani kwake London mashariki kuelekea Syria na marafiki wawili wa shule mwaka 2015 na akiwa huko, aliolewa na mpiganaji wa kundi la IS.