Mvutano waibuka upya Sudan
23 Mei 2011Matangazo
Katika taarifa iliyotolewa Khartoum, mji mkuu wa Sudan, wajumbe wa Baraza la Usalama, wameelezea wasiwasi wao kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya katika eneo la Abyei. Siku ya Jumamosi, wanajeshi wa kaskazini walilidhibiti eneo hilo linalogombewa na Sudan ya Kaskazini na Kusini.Kura ya maoni iliyopangwa kufanywa mwezi wa Januari kuamua hatima ya eneo hilo la mpakani lenye utajiri wa mafuta, imeahirishwa kwa sababu ya hali ya mvutano na matatizo ya mipangilio.
Mwezi huo wa Januari, katika kura ya maoni iliyopigwa Sudan ya Kusini, wakaazi wake waliamua kujitenga na Kaskazini. Taifa huru la Sudan ya Kusini linatazamiwa kutangazwa rasmi tarehe 9 Julai, ikiwa ni miaka sita baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan.