1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mukwege ahimiza mapambano dhidi ya udhalilishaji wa ngono

Josephat Charo
3 Juni 2021

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Denis Mukwege, amewahimiza wanasiasa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kujihusisha na mapambano dhidi ya udhalilishaji wa ngono na mauaji ya raia mashariki mwa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/3uNtQ
Demokratische Republik Kongo | Besuch Heiko Maas bei Denis Mukwege, Friedensnobelpreisträger
Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Daktari huyo raia wa Congo ambaye ni bingwa wa upasuaji na masuala ya wanawake alikuwa amealikwa na spika wa bunge la mkoa wa Kivu Kusini kuwahutubia wabunge kuhusu suala la unyanyasaji kingono na utumiaji wa ubakaji kama silaha ya vita nchini Congo.

Mukwege alisema kujitolea kwa dhati kwa viongozi wa kisiasa katika ngazi ya majimbo na kitaifa kumekosekana katika mapambano dhidi ya machafuko mashariki mwa taifa hilo.

SOma pia: Asasi za kiraia DRC zalaani vitisho dhidi ya Mukwege

Matamshi ya Mukwege yamekuja siku moja baada ya serikali ya Congo mjini Kinshasa kuapa kuharakisha kampeni ya usalama eneo la mashariki, ambako mamia ya watu wameuliuwa na makundi ya waasi tangu mwanzoni mwa mwaka huu.