Asasi za kiraia DRC zalaani vitisho dhidi ya Mukwege | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.08.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Asasi za kiraia DRC zalaani vitisho dhidi ya Mukwege

Asasi za kiraia za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zautaka Umoja wa Mataifa kuwafuatilia watuhumiwa katika ripoti ya Mapping ya mwaka 2010 iliyotokana na uchunguzi wa wataalamu wa umoja huo juu ya mauaji na uhalifu DRC.

Aidha, asasi hizo zinalaani vitisho vinavyotolewa dhidi ya mshindi wa tuzo ya Nobel Dokta Denis Mukwege aliyekuwawa kwanza kukumbushia kuhusu ripoti hiyo ya mauaji na hasa mashariki mwa Kongo.

Vitisho dhidi ya Daktari Denis Mukwege vinafuatia kukemea kwake mauaji yaliyofanyika katika kijiji cha Kipupu katika wilaya ya Mwenga mkoani Kivu Kusini Julai 16 mwaka huu, ambapo watu wengi waliripotiwa kuuawa na wapiganaji wa makundi yenye silaha.

Mshindi wa Nobel

Mukwege ambaye ni mshindi wa tuzo la amani ya Nobel mnamo mwaka 2018 ametaka mapendekezo ya ripoti ya ya Mapping iliyochapishwa na kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa mnamo Oktoba 2010, ili kuwawajibisha waliohusika katika uhalifu uliotendwa nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo tangu wa elfu moja mia tisa tisini na sita (1996). Mukwege pia alisisitiza wito wake wa kuundwa kwa mahakama maalum ili kuhumuku uhalifu huo.

Katika mkutano na wanahabari mjini Bukavu siku ya Ijumaa, wanaharakati wa asasi za kiraia, akiwemo Profesa Arnold Nyaluma wanaunga mkono juhudi za Daktari Denis Mukwege, na kuuhimiza umoja wa mataifa utekeleze mapendekezo ya ripoti hiyo miaka kumi baadae.

Kilicho kera zaidi ni pale Mukwege alipobaini kwamba wanaotenda mauaji ni watu walewale ambao wameendelea kuuwa tangu mwaka 1996, kwa sababu bado wako huru na wanafurahia hali ya kutoadhibiwa iliyotawala nchini DRC.

Ruanda Verteidigungsminister James Kabarebe in Kigali

Jenerali James Kabarebe, mshauri mkuu wa Rais Paul Kagame kuhusu masuala ya usalama

Raphael Wakenge ni kiongozi wa shirika la ICJP, analalamikia hali ya kuwa baadhi ya watuhumiwa wako kwenye ngazi za juu za uongozi. Anataka orodha ya majina yao itangazwe na pia kuundwe sheria ya mpito:

Kiongozi wa shirika la raia katika mkoa wa Kivu Kusini, Marie Migani amesisitiza kwamba raia wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo watazidi kupiga mbiu hadi pale sauti zao zitakapo sikika ili wahanga wa uhalifu watendewe haki.

Mukwege atuhumiwa

Akijibu swali lililoulizwa na raia wa Rwanda anayeishi nchini Cameroun wakati wa matangazo kwenye Televisheni ya Kitaifa ya Rwanda mnamo Julai 18, waziri wa zamani wa ulinzi wa Rwanda ambaye sasa ni mshauri mkuu wa Rais Paul Kagame kuhusu masuala ya usalama, Jenerali James Kabarebe alimtuhumu Dokta Mukwege kwa kutumia ripoti ya Mapping pamoja na watu wengine aliowaelezea kuhusika na mauaji ya kimbari, kutengeneza propaganda zinazokiuka ukweli wa mambo.

Jenerali Kabarebe alisema iweje mamilioni ya watu hao wote wanaweza kuuawa bila kuona hata mwili mmoja. Amesema kwamba jeshi la Rwanda halikumuua mtu yeyote nakwamba wakati huo jeshi hilo lilikuja Congo kuwaokoa wakimbizi wa Rwanda waliokuwa wametekwa nyara, na kuhitimisha kuwa madai mengine yoyote hayana maana.

Marekani na Canada zimelaani vitisho dhidi ya Dokta Mukwege na kutaka hali ya kutoadhibiwa ikomeshwe kutokana na ghasia ziliyofanyika mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.