1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Daktari Denis Mukwege Mukengere

Denis Mukwege ni mtaalamu wa magonjwa ya wanawake na mchungaji wa Kanisa la Kipentekosti. Alianzisha na anafanya kazi Hospitali ya Panzi iliyopo mjini Bukavu ambapo anajikita katika kuwatibu wanawake waliobakwa na waasi.

Mwaka 2018, Mukwege kwa pamoja na mwanaharakati wa haki za binadamu wa Kiyazidi Nadia Murad, walitunukiwa tuzo ya Nobel kutokana na juhudi za kukomesha vurugu za kingono kama silaha ya kivita pamoja na migogoro ya silaha. Ukurasa unakusanya maudhui za DW kuhusu Dk. Denis Mukwege.