1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshindi wa medali ya mashindano ya dunia Kenya Tirop afariki

13 Oktoba 2021

Shirika la Riadha nchini Kenya AK, limesema kuwa mshindi mara mbili wa nishani ya shaba ya riadha Agnes Jebet Tirop, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 25, katika tukio linalodaiwa kuwa la mauaji.

https://p.dw.com/p/41dUj
Langstreckenläuferin aus Kenia Agnes Jebet Tirop
Picha: Fredrik Sandberg/TT NYHETSBYRÅN/picture alliance

Tirop alikutwa nyumbani kwake Iten akiwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali, kwa mujibu wa Riadha Kenya na ripoti za vyombo vya habari.

Tirop alishinda medali ya shaba ya dunia katika mbio za mita 10,000 mwaka 2017 na 2019, na alimalizia nafasi ya nne katika mbio za mita 5,000 za mashindano ya Olimpiki ya Tokyo zilizofayika Japan mwaka huu.