Mpiga kura kutojitokeza licha ya kufuatwa kwa helikopta na IEBC | Masuala ya Jamii | DW | 09.08.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mpiga kura kutojitokeza licha ya kufuatwa kwa helikopta na IEBC

Licha ya IEBC kupeleka maafisa wake kwa helicopta kumfuata mpiga kura pekee katika kituo cha LochorApua, Loitamoe Eripon, alishindwa kujitokeza kupiga kura yake.

Mpigaji kura nchini Kenya, Loitamoe Eripon, ambaye alikuwa ni mtu pekee aliyejiandikisha kupiga kura katika kituo cha LochorApua, Jimbo la Turkana Magharibi, hakujitokeza kutimiza haki yake ya kikatiba, Jumanne siku ya uchaguzi mkuu. Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka Kenya IEBC ambao walitembelea kituo hicho kwa kutumia usafiri wa helikopta ili kuhakikisha Eripon anatimiza haki yake ya kikatiba ilibidi warudi walipotoka kwa sababu bwana huyo hakujitokeza kupiga kura kituoni. Jimbo la Turkana Magharibi linapakana na nchi jirani ya Sudan Kusini.

Mwandishi: Yusra Buwayhid

Mhariri:Iddi Ssessanga

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com