1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAlgeria

Moto mkubwa wateketeza msitu mpakani mwa Algeria

21 Julai 2023

Maafisa wa zimamoto nchini Tunisia wanapambana kuuzima moto mkubwa ambao umezuka kwa siku mbili katika msitu ulioko karibu na mpaka na Algeria.

https://p.dw.com/p/4UEL8
Unwetter extrem weltweit Update für BG Algerien
Picha: ABDELAZIZ BOUMZAR/REUTERS

Mamlaka katika eneo hilo wanasema ekari 1,100 za msitu tayari zimeteketea kwa moto huku askari wa zimamoto pamoja na helkopita ya kijeshi wakiendelea kupambana kuukabili moto huo.

Soma pia: Miili ya wahamiaji yapatikana kwenye mpaka wa Tunisia-Algeria

Moto huo umesababisha kivuko cha mpaka cha kuingia Algeria cha Malloula kufungwa kwa muda kutokana na moshi mzito. Familia kadhaa zimeondolewa kutoka eneo lililoathirika karibu na mji wa mapumziko wa Tabarka kwenye bahari ya Mediterenia.

Soma pia: Moto waua watu 50 Ugiriki

Hakuna mtu aliyejeruhiwa katika mkasa huo. Kama ilivyo kwa nchi nyingine zilizo kanda ya bahari ya Mediterenia, Tunisia inakabiliwa na wimbi la joto kali.