MOSCOW : Moto mwengine wazuka hospitali | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW : Moto mwengine wazuka hospitali

Moto uliozuka kwenye hospitali moja karibu na mji wa Siberia wa Kemerovo umeuwa watu tisa na kujeruhi wengine 16 wakati wa usiku.

Huo ni moto wa pili kuzuka nchini Urusi katika hospitali mwishoni mwa juma hili.Maafisa wanasema wakati moto huo ulipowaka kwenye hospitali hiyo ya magonjwa ya akili na mishipa ya fahamu ya jengo la ghorofa mbili kulikuweko na watu 325 pamoja na wafanyakazi wa matibabu 15.

Moto huo uliozuka usiku wa kuamkia leo unafuatia ule uliozuka hapo Jumamosi katika hospitali ya kutibu wagonjwa wa madawa ya kulevya mjini Moscow ambapo wanawake 45 waliuwawa na inashukiwa kwamba moto huo ulitokana na hujuma.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com