1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Lugovoi asema hakumuua Litvinenko

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwK

Aliyekuwa jasusi wa shirika la ujasusi la Urusi ya zamani, KGB, Andrei Lugovoi, anayeshukiwa kwa mauaji ya Alexander Litvinenko, amesema shirika la ujasusi la Uingereza lilitaka kumwajiri.

Andrei Lugovoi, aliyekuwa akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjijni Moscow, amesema Litvinenko hakuwa adui yake na kwamba anasingiziwa kwamba ndiye aliyemuua.

Juma lililopita serikali ya Uingereza iliitolea wito Russia kumrejesha Lugovoi ili akajibu mashtaka ya mauaji ya Alexander Letvinenko.

Bunge la Russia limesema katiba ya nchi hiyo hairuhusu mshukiwa huyo kurejeshwa Uingereza.

Alexander Letvinenko, aliyekuwa afisa wa kijasusi wa KGB, alifariki dunia mjini London mwaka uliopita kutokana na miale ya sumu.