MOGADISHU:Saba wauwawa Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 09.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU:Saba wauwawa Somalia

Mirupuko kadhaa imetikisa mji mkuu wa Somalia Mogadishu.Wanamgambo wameripua maguruneti dhidi ya vikosi vya wanajeshi wa serikali katika soko la Bakara mjini humo.Wanajeshi hao wamelipiza mashambulio hayo kwa kufyatua risasi na kusababisha kuwawa kwa raia saba .

Wakaazi wa eneo hilo wanasema wengi wengine wamejeruhiwa kwenye mashambulio hayo ya risasi katika wilaya za Hawlwadag na Wardhigley kusini mwa mji wa Mogadishu ambako polisi wamekuwa wakishika doria.

Wakati huohuo lori lililokuwa limewabeba watu kadhaa waliokuwa wakikimbia vita mjini Mogadishu lilipinduka na kuua zaidi ya watu 16.

Kwa siku mbili mfululizo mji wa Mogadishu umekumbwa na ghasia na wanajeshi wa Somalia na Ethiopia wanasema soko la wazi la Bakara ndio maficho makubwa ya wanamgambo wakiislamu ambao wamezidisha kutumia mbinu zinazofanana na zile zinazotumika Iraq kufanya mashambulio ikiwa ni pamoja na kuua watu kutega mabomu kandoni mwa barabara na kujitoa muhanga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com