MOGADISHU: Mripuko sokoni umeua watu 3 Somalia
18 Julai 2007Matangazo
Majadiliano ya amani yanayotazamiwa kufanywa nchini Somalia yamegubikwa na shambulizi la gruneti lililofanywa sokoni katika mji mkuu Mogadishu.Shambulizi hilo limefanywa siku moja kabla ya kufunguliwa mkutano wa amani mjini Mogadishu na limeua si chini ya watu watatu,ikiwa ni pamoja na mwanajeshi mmoja.Mkutano huo uliahirishwa siku ya Jumamosi katika hali ya machafuko.Raia 4 pia waliuawa katika mripuko uliotokea katika soko hilo hilo siku ya Jumanne.