MOGADISHU: Miripuko yatokea Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 02.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Miripuko yatokea Somalia

Miripuko kadhaa imetokea mjini Mogadishu nchini Somalia hii leo siku moja baada ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kuwasili nchini humo.

Wakaazi wa Mogadishu wamesema wamesikia makombora yakivurimishwa kuelekea bandari ya mjini Mogadishu. Ripota aliyeshuhudia amesema makombora matatu yalianguka katikati mwa jiji la Mogadishu na kuuharibu mkahawa, nyumba moja na basi ya abiria. Amesema watu sita wamejeruhiwa kufuatia shambulio hilo.

Hujuma hiyo imefanywa siku moja baada ya watu waliokuwa na bunduki kuwapiga risasi na kuwaua watu watatu katika nyumba ya mkurugenzi wa bandari ya Mogadishu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com