Mkutano wa nchi wanachama wa G7 waanza leo nchini Ufaransa
15 Juni 2026
Washirika hao wa G7 watataka kupata maelezo zaidi kuhusu makubaliano hayo pamoja na mpango wa kufungua tena Mlango-Bahari wa Hormuz kwa shughuli za usafirishaji wa meli.
Hata hivyo, suala la Iran halitakuwa la pekee lenye mvutano katika mkutano huo wa siku tatu. Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, anatarajiwa kuhudhuria kuanzia kesho Jumanne, kufuatia mashambulizi makali ya hivi karibuni yaliyofanywa na Urusi dhidi ya Ukraine, ambayo yalisababisha moto katika kanisa kuu la kihistoria jijini Kyiv.
Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa Instagram, mwenyeji wa mkutano huo ambaye ni rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, amesema mkutano huo utachunguza matokeo ya makubaliano ya Iran, ambayo yanatarajiwa kutiwa saini nchini Uswisi Ijumaa, hasa kuhusu athari zake kwa Lebanon, kufunguliwa kwa kudumu kwa ujia wa bahari wa Hormuz, na shughuli za Iran zinazohusiana na makombora .