1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkurugenzi wa Human Rights Watch atangaza kujiuzulu

Zainab Aziz
26 Aprili 2022

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch amesema kuwa atauachia wadhifa huo mwishoni mwa mwezi Agosti.

https://p.dw.com/p/4ARw0
Human Rights Watch | Kenneth Roth
Picha: Johannes Eisele/AFP/Getty Images

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kutetea haki za binadamu, Human Rights Watch, Kenneth Roth, amesema leo kuwa atauachia wadhifa huo mwishoni mwa mwezi Agosti baada ya kuliongoza shirika hilo kwa karibu miongo mitatu.

Human Rights Watch imesema itaanza mkakati wa kumpata mrithi wa Roth, na kwamba naibu wake, Tirana Hassan, atahudumu kama mkurugenzi mtendaji wa muda wa shirika hilo linalofuatilia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote.

Roth, alijiunga na shirika la Human Rights Watch mnamo mwaka 1987 kama naibu mkurugenzi na kisha kupanda cheo. Amesema ataandika kitabu juu ya uzoefu wake binafsi kuhusu mikakati madhubuti zaidi ya kutetea haki za binadamu.