1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misri: Watu wanne wauawa kufuatia shambulizi la kanisa

29 Desemba 2017

Watu wanne wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na wanaoshukiwa kuwa wanamgambo dhidi ya kanisa la madhehebu ya Coptic mjini Cairo siku ya Ijumaa.

https://p.dw.com/p/2q5rw
Ägypten Helwan Anschlag auf Mar Mina Kirche
Picha: Reuters/A. Abdallah Dalsh

Watu wanne wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na wanaoshukiwa kuwa wanamgambo dhidi ya kanisa la madhehebu ya Coptic mjini Cairo siku ya Ijumaa.

Washambuliaji wawili waliwafyatua risasi kwa polisi waliokuwa wakilinda eneo hilo la kuabudia katika kitongoji cha Helwan kilichoko mashariki mwa Cairo na kumuua mfanyakazi wa kanisa na polisi watatu.

Polisi baadae walimuua mshambuliaji mmoja lakini mshambuliaji wa pili alifanikiwa kutoroka. Katika miezi ya hivi karibuni, wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali wamezidisha mashambulizi katika makanisa hayo nchini Misri.

Mwezi Desemba mwaka jana, watu 25 waliuawa katika shambulio la kujitoa muhanga, kwenye kanisa kuu mjini Cairo. Mwezi Aprili, mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga wakati wa ibada ya jumapili ya matawi kwenye makanisa mawili ya Coptic yaliwaua watu 47, na kuichochea Misri kutangaza hali ya hatari nchi nzima.