Miaka mitano tangu kutokea Tsunami, Ibada zafanyika duniani kote. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 27.12.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Miaka mitano tangu kutokea Tsunami, Ibada zafanyika duniani kote.

Ibada ya maombi kuwakumbuka wahanga takriban laki mbili waliofariki kufuatia janga lililosababisha maafa mabaya kabisa ya Tsunami imefanyika katika maeneo mbali mbali duniani.

Watu walionusurika na janga la Tsunami nchini Sri Lankan wakifanya ibada ya kuwakumbuka wahanga.

Watu walionusurika na janga la Tsunami nchini Sri Lankan wakifanya ibada ya kuwakumbuka wahanga.

JAKARTA

Ibada ya maombi kuwakumbuka wahanga takriban laki mbili , waliofariki kufuatia janga lililosababisha maafa mabaya kabisa la Tsunami katika bahari ya hindi miaka mitano iliyopita- imefanyika katika maeneo mbali mbali kote ulimwenguni. Desemba tarehe 26, mwaka wa 2004, mawimbi makubwa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililokuwa katika kiwango cha 9.2 katika kipimo cha Richter chini ya bahari, liliathiri nchi 13 barani Asia na nchi zilizo katika pwani ya Afrika. Ibada ya kumbukumbu ilifanyika jana huko nchini Indonesia, Sri Lanka, India na Thailand. Hapa Ujerumani ibada hiyo ilifanyika katika mji wa Dusseldorf. Zaidi ya Wajerumani 550 waliokuwa likizoni walifariki au walipotea kufuatia mkasa huo wa Tsunami.

 • Tarehe 27.12.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/LEFv
 • Tarehe 27.12.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/LEFv
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com