Mgogoro wa nyuklia wa Fukushima wachacha | Masuala ya Jamii | DW | 21.08.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Mgogoro wa nyuklia wa Fukushima wachacha

Mamlaka ya udhibiti wa nishati ya nyuklia nchini Japan, imesema mgogoro wa nyuklia wa nchi hiyo umefikia kiwango kibaya zaidi katika kipindi cha miaka miwili, huku China ikielezea kushtushwa na baa hilo.

This photo taken on August 6, 2013 shows local government officials and nuclear experts inspecting a construction site to prevent the seepage of contamination water into the sea, at Tokyo Electric Power's (TEPCO) Fukushima Dai-ichi nuclear plant in Okuma, Fukushima prefecture. Japan will accelerate efforts to prevent more radioactive groundwater from seeping into the ocean at the crippled Fukushima nuclear plant, government officials said on August 7, as critics slam its operator's handling of the issue. JAPAN OUT AFP PHOTO / JAPAN POOL via JIJI PRESS (Photo credit should read JAPAN POOL/AFP/Getty Images)

300 Tonnen radioaktives Wasser versickert in Fukushima August 2013

Mamlaka ya nyuklia ya Japan NRA, pia imesema kuwa inahofia kuwa baa hilo limezidi uwezo wa kampuni inayoendesha mitambo ya nyuklia ya Tokyo Electric Power Co, Tepco, kukabiliana na mgogoro huo. Msemaji wa NRA amesema mapema leo kuwa mamlaka hiyo inapanga kupandisha ukubwa wa mgogoro huo kutoka kiwango cha kwanza cha tahadhari, ambacho kinawakilisha jambo lisilo la kawaida, hadi kiwango cha tatu kinachowakilisha tukio zito, katika vipimo vya kimataifa vya rediolojia.

Mfanyakazi akiwa mbele ya matangi ya kampuni ya Tepco.

Mfanyakazi akiwa mbele ya matangi ya kampuni ya Tepco.

Hatua kama hiyo itakuwa ndiyo nzito zaidi kuwahi kuchukuliwa tangu kiwanda cha nyuklia cha Japan kilipoharibiwa kufuatia tetemeko la ardhi na tsunami mwaka 2011. Waziri wa nchi anaeshughulika na masuala ya baraza la mawaziri Yoshihide Suga hali ya mtambo huo ni ya kusikitisha, na kwamba serikali itafanya kila juhudi kukomesha kuvuja maji yaliyochafuliwa haraka iwezekanvyo.

China yashtushwa
Kampuni ya umeme ya Japan Tepco ilisema siku ya Jumanne kuwa maji yenye viwango vikubwa vya rediolojia yanavuja kutoka tangi la kuhifadhia, huku NRA nayo ikisema kuwa ina wasiwasi kuhusu uvujaji kutoka matangi mengine ya aina hiyo, ambayo yalijengwa haraka haraka kuhifadhi maji yanayotumika kupoozea mitambo ya kituo hicho. China ilisema katika taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni, kuwa imeshtushwa na habari za kuendelea kuvuja kwa mtambo wa fukushima, miaka miwili baada ya ajali, na kuisihi Japan kutoa taarifa kwa wakati na kupitia njia zinazostahiki.

Maji yanayovuja kwa sasa yana kiwango kikubwa cha sumu kiasi kwamba mtu akisimam karibu na tangi hilo kwa saa moja anaweza kupata mara tano zaidi ya kiwango cha juu kinachopendekezwa kwa wafanyakazi wa nyuklia katika kipindi cha mwaka mmoja.

Meneja Mkuu wa Tepco, Masayuki Ono.

Meneja Mkuu wa Tepco, Masayuki Ono.

"Kipmo cha Millissivert mia moja kwa saa ni sawa na kiwango cha juu cha mwisho katika kipindi cha miaka mitano kwa wafanyakazi wa nyuklia. Kwa hivyo tumegundua viwango vya rediolojia vyenye uwezo wa kumpa mtu dozi ya rediolojia ya miaka mitano ndani ya saa moja," amesema Masayuki Ono, meneja mkuu wa kampuni ya umeme ya Tepco.

Kupandishwa kwa kiwango cha tatu cha tahadhari ndiyo mara ya kwanza kwa Japan kutoa onyo kwa vipimo vya shughuli za kimataifa za nyuklia, INES, tangu mitambo mitatu ilipoanza kuvuja, baada ya tetemeko kubwa na tsunami mwaka 2011. Kila ongezeko la hatua moja ya INES linawakilisha ongezeko mara kumi ya ukalifu, kwa mujibu wa taarifa iliyopo katika mtandao wa shirika la atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA.

Mwandishi: Iddi Ismail Ssessanga/rtre
Mhariri: Saum Yusuf

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com