1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSaudi Arabia

Mfalme Salman aongoza mkutano wa baraza la mawaziri

28 Mei 2024

Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia Jumanne ameongoza mkutano wa baraza la mawaziri katika taifa hilo la utawala wa kifalme.

https://p.dw.com/p/4gO7L
Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia
Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia Picha: Andrew Caballero-Reynolds/REUTERS

Hii ni mara ya kwanza kwa mfalme huyo kutekeleza majukumu rasmi ya kiserikali tangu alipotibiwa zaidi ya wiki moja iliyopita.

Mfalme Salman alionekana kwenye picha akiongoza mkutano huo wa kila wiki wa baraza la mawaziri uliofanyika kwa njia ya video. Mwanamfalme Mohammed bin Salman, akiwa pamoja na mawaziri, pia alihudhuria mkutano huo.

Salman bin Abdulaziz mwenye umri wa miaka 88 alitawazwa kuwa mfalme wa nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta mnamo mwaka 2015. Kabla ya hapo, alihudumu kama naibu waziri mkuu.