Messi aifikia rekodi ya Ligi ya Mabingwa | Michezo | DW | 07.11.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Messi aifikia rekodi ya Ligi ya Mabingwa

Lionel Messi alifunga mabao mawili dhidi ya Ajax katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, na kufikisha 71 idadi ya magoli yake katika dimba hilo, sawa na rekodi iliyowekwa na Raul. Cristiano Ronaldo na magoli 70

Messi mwenye umri wa miaka 27, ambaye pia ni mfungaji wa magoli mengi katika klabu ya Barcelona, huenda hata hivyo asiweze kuishikilia rekodi hiyo kwa muda. Inaonekana kuwa ni suala la muda tu, (labda wiki mbili) ambapo Messi atafunga goli lake la 72 na kumpiku Raul, lakini mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo tayari ana magoli 70. Nyota huyo Mreno, mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka, alikuwa mfungaji bora wa dimba hilo katika msimu uliopita.

Messi na Ronaldo hutawala chati za ufungaji magoli katika ligi ya Uhispania na pia kura za kila mwaka za kimataifa za tuzo ya mchezaji bora ulimwenguni. Huku wakichezea vilabu viwili bora zaidi barani Ulaya, na wote wakiwa chini ya kidogo ya umri wa miaka 30, ni vyema kusema kuwa wataweza kutikisa nyavu mara kadhaa katika dimba hilo la Ulaya.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Rueters
Mhariri: Sekione Kitojo