Merkel: Mzozo wa wahamiaji watishia mkataba wa Schengen | Matukio ya Kisiasa | DW | 31.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Merkel: Mzozo wa wahamiaji watishia mkataba wa Schengen

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema mzozo wa wahamiaji wanaoingia Ulaya ni jaribio kubwa kwa misingi ya Umoja wa Ulaya inayohimiza usawa kwa wote. Merkel pia ameonya kuwa tatizo hilo litakuwepo kwa muda mrefu.

Wakimbizi wakimiminika katika kituo cha treni nchini Hungary

Wakimbizi wakimiminika katika kituo cha treni nchini Hungary

Hayo Kansela Angela Merkel ameyasema leo mjini, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa kimataifa. Amesema ikiwa nchi za Umoja wa Ulaya hazitakuwa tayari kushirikiana kubeba mzigo wa wakimbizi, basi suala la msingi la uswa kwa wote ambalo Umoja wa Ulaya umejengwa juu yake litakuwa halipo tena.

Mapema Ujerumani , Ufaransa na Uingereza zimeweka mkazo katika umuhimu wa kushughulikia sula ala wakimbizi wanaoingia katika nchi za ulaya ya kusini na pia haja ya kuwa na orodha ya mataifa ambayo wakimbizi wanatoka na yasiyokabiliwa na migogoro huku pia mataifa hayo yakipendekeza kuitishwa kwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani na sheria wa Umoja wa Ulaya septemba 14 mwaka huu.

Maeneo maalum kwa wakimbizi

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani

Mawaziri wa mambo ya ndani, Thomas de Maiziere wa Ujerumani, Bernard Cazeneuve wa Ufaransa na Theresa May wa Uingereza walisisitiza umuhimu wa kuweka maeneo ya hatari katika mataifa ya Ugiriki na Italia kufikia mwishoni mwa mwaka huu ili kuhakikisha kuwa wahamiaji wanachukuliwa alama za vidole na kusajiliwa ili kuweza kuwabaini wale hasa wanaohitaji kulindwa na kupewa hifadhi.

Katika taarifa yao mawaziri hao walishauri kuitishwa kwa kikako cha mawaziri wa mabo ya ndani ili kujadili suala hilo. De Maiziere alisema ya kuwa umoja wa ulaya haipaswi kusubiri hadi siku ya mkutano uliopangwa mapema mwezi Oktoba mwaka huu kujadili suala hilo na tayari Luxembourg ambayo inashikilia urais wa kupokezana wa umoja wa ulaya imetoa taarifa yake kupitia mtandao wa twitter ya kuwa mawaziri hao wa mamboo ya ndani na sheria watakutana septemba 14 mwaka huu ili kujadili jinsi ya kuboresha mikakati ya kushughulikia masuala ya wakimbizi.

Ujerumani ambayo imekuwa ikipokea maombi mengi ya wahamiaji wanao omba hifadhi ya kisiasa kutoka katika mataifa ya Balkan inasisitiza juu ya suala la kuwa na orodha ya mataifa yaliyosalama ili kurahisisha zoezi la kuwarejesha wakimbizi makwao ambao wataonekana hawana haja ya haja kupatiwa hifadhi ya kisiasa.

" Hii itasaidia kuwapa hifadhi wale wenye mahitaji na pia ni lazima tuwaeleze wale ambao hawana umuhimu wa kupewa hifadhi kuwa hawawezi kuka nasisi." Alisema Kansela Angel Merkel hapo jana mjini Berlin.

Aliongeza kuwa wale ambao awanahitaji kulindwa ni lazima wapatiwe hifadhi haraka lakini wale wanaonekana hawasitahili lazima warejeshwe makwao haraka.

Ujerumani kupokea wakimbizi 800,000

Mzozo wa wakimbizi umezigawa kimaoni nchi za Umoja wa Ulaya

Mzozo wa wakimbizi umezigawa kimaoni nchi za Umoja wa Ulaya

Wakimbizi wanaotarajiwa kuingia nchini Ujerumani kwa mwaka huu idadi yao inakisiwa kufikia 800,000 ikiwa ni mara nne zaidi ya mwaka jana.

Aidha Ujerumani inayataka mataifa mengineyo katika umoja wa ulaya kukubali pia kupokea wakimbizi ili kuipunguzia mzigo tofauti na inavyo onekana sasa.

Wakati huohuo Hungaryhapo jana imeshutumu kauli iliyotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius kuhusiana na kauli yake ya kukosoa juu ya hatua ya nchi hiyo ilizochukuwa za kujenga uzio mrefu wa senyenge katika mpaka wake na Serbia ili kuwadhibiti wakimbizi wasiweze kuingia kirahisi katika taifa hilo.

Katika mahojiano na Radio Ufaransa hapo jana Fabius alisema hatua hiyo ya Hungary ya kujenga uzio inakwenda kinyume na maadili ya mataifa ya ulaya.

Hii inamaanisha Hungary haiheshimu maadili ya pamoja ya mataifa ya ulaya hivyo umoja wa ulaya inabidi uwe na majadiliano mazito na maafisa wake kuhusiana na na suala la wakimbizi.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Hungary Peter Szijjarto alisema ya kuwa badala ya mtu kutoa kauli zisizo na msingi za kulaumu anapaswa kuzingatia zaidi juu ya kupatikana kwa suluhusho la pamoja kuhusiana na suala hilo la wakimbizi. Akionekana kupinga matamshi hayo ya waziri wa mabo ya nchi za nje wa Ufaransa Laurent Fabius.

Mwandishi: Isaac Gamba/APE/AFPE

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman

DW inapendekeza

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com