Melbourne. Mto mkubwa unawaka msituni. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Melbourne. Mto mkubwa unawaka msituni.

Maafisa nchini Australia wanajaribu kuudhibiti moto mkubwa kabisa katika historia ya nchi hiyo unaowaka msituni .

Vikosi vya jeshi vimetumwa hivi sasa kusaidia wazima moto kupambana na moto huo katika jimbo la Victoria jimbo ambalo ndio limeathirika kwa kiasi kikubwa na mto huo.

Moshi mkubwa umezingira mji wa Melbourne, mji wa pili kwa ukubwa nchini Australia na kuzuwia usafiri wa anga na kusababisha ving’ora vya tahadhari kulia katika uwanja wa ndege.

Kiasi cha hekta 180,000 za ardhi tayari zimeharibiwa na moto huo na maafisa wanahofia kuwa kiasi cha hekta 600,000 zinaweza kuharibiwa katika muda wa siku zijazo. Wazima moto wanasema mto wa misituni wa msimu huu umeongezwa kasi na hali mbaya ya ukame.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com