Mbunge wa Hezbollah azituhumu nchi za Kiarabu kuwa vibaraka | Matukio ya Kisiasa | DW | 25.06.2020
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mbunge wa Hezbollah azituhumu nchi za Kiarabu kuwa vibaraka

Mbunge wa Hezbollah nchini Lebanon, Ibrahim Mousawi amezituhumu nchi za Kiarabu kuwa vibaraka vya Marekani. Mousawi amesema mzozo wa kisiasa nchini mwake utaendelea ikiwa Wamarekani hawatositisha njama zao. 

Kwenye mahojiano ya kipekee na kituo cha televisheni cha DW/TV, msemaji wa kundi la Hezbollah ambae pia ni mbunge wa kundi hilo, Ibrahim Mousawi amesema kwamba kundi lao ni vuguvugu la upinzani dhidi ya adui.

"Ukija nchini Lebanon,utakuta mamilioni ya watu wakiunga mkono kesi yetu.Sisi ni kundi la upinzani dhidi ya adui, linalo pigana kwa ajili ya ukombozi wetu kutokana na uvamizi wa Israel ilikukinga nchi yetu".

Mousawi amesema kwamba vita vyao vya kupinga uvamizi na kwa ajili ya uhuru wa kiuchumi vinasababisha wapachikwe majina na Marekani. Huku akielezea kwamba nchi nyingi za Kiarabu ni vibaraka vilivyo mkono mwa Marekani.

Akigusia mzozo wa kisiasa na kutofaulu kwa mageuzi nchini mwake, kufuatia maandamano ya miezi iliopita, Mousawi amesema kwamba wanasiasa wote wanatakiwa kubeba dhamana ya kile kilichotokea nchini Lebanon.

Je kuna ukosefu wa nia nzuri kutekeleza mageuzi ya kisias ana kiuchumi?

"Kila mtu anawajibika. Na sisi hatukanushi wajibu huo",Mousawi amesema.

Mbunge huyo alikuwa akiyajibu madai ya mshauri wa wizara ya fedha ya Lebanon, Henri Chaoul, aliyeelezea ukosefu wa nia nzuri ya kisiasa katika utekelezwaji wa mageuzi ya kisiasa na kiuchumi.

"Tulitekeleza majukumu yetu kwa kuishinikiza serikali kufanya mageuzi.Tuko tayari kuchukuwa majukumu yetu na tunawajibika kwa hilo. Lakini tulichukuwa pia majukumu ya kupambana na makundi ya Takfiri mpakani mwa Lebanon na vilevile uvamizi wa Israel",amesema Mousawi.

Kuhusu vita dhidi ya rushwa nchini Lebanon,Ibrahim Mousawi anasema kwamba kundi lake la Hezbollah linachukulia swala hilo kama moja wapo ya vipaumbele.Na kundi hilo halijaunga mkono mtu aliejihusisha na rushwa.

Waandamanaji katika mji mkuu wa Lebanon kupinga kudorora kwa uchumi. (Picha ya maktaba)

Waandamanaji katika mji mkuu wa Lebanon kupinga kudorora kwa uchumi. (Picha ya maktaba)

Hezbollah yakanusha kushambulia waandamanaji

Msemaji wa kundi la Hezbollah alikanusha mashambulizi ya kundi lake dhidi ya waandamanaji wakati wa maandamano ya hivi karibuni nchini Lebanon.

Anasema kwamba wao sio miongoni mwa wale wanaogandamiza raia.

"Tuko pamoja na raia.Tulifurahi kuona watu wanaandamana kwa kupinga rushwa.Kuna makundi yaliochukuwa nafasi hiyo kwa ajili ya kuendesha agenda zao za kisiasa. Na hapo ndipo vikosi va usalama vilingilia kati"aliendelea kusema Mousawi.

Ibrahim Mousawi anasema kwamba Lebanon ni mhanga wa Marekani ambayo inaunga mkono Israel kwa kukanyaga haki za watu wa Palestina wa kuwa na taifa huru.

Shirika la kupambana na mihadarati: Hezbollah yafaidika kwa njia ya uhaini

Alipohojiwa kuhusu ripoti ya shirika la Drug Enforcement Agency, ambayo inaelezea kwamba kundi la Hezbollah inategemea zaidi pato za njia ya uhaini, Mousawi alisema kwamba madai hayo yametungwa kwa ajili ya vyombo vya habari vya nchi za magharibi dhidi ya Hezbollah,ilikuikashifu na sababu za kuiwekea vikwazo.

Msemaji wa kundi la Hezbollah,Ibrahim Mousawi anasema kwamba mzozo nchini Lebabon utaendelea endapo Wamarekani wataendelea na njama zao. Lakini anathibitisha kwamba Lebano haitaingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.