1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Kuleba kuzuru India katika juhudi za kuimarisha ushirikiano

Tatu Karema
27 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba Alhamisi ataanza ziara ya siku mbili nchini India ambapo atajadili masuala ya kimataifa. Haya yametangazwa leo na wizara ya Mambo ya Nje ya India.

https://p.dw.com/p/4eBe0
Ujerumani I Heiko Maas akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Heiko Maas, mjini Berlin, Ujerumani, Jumatano Juni 9, 2021.Picha: John Macdougall/AP/picture alliance

Wizara ya Mambo ya Nje imesema kuwa Kuleba, atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India S. Jaishankar mjini New Delhi na pia akitarajiwa kufanya mazungumzo na mshauri msaidizi wa masuala ya usalama wa taifa  wa India.

Taarifa hiyo imesema Kuleba atajadili kuhusu ushirikiano katika masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi kwa mataifa hayo mawili.

India imejiepusha na shutuma za wazi za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine hata, baada ya kutafuta ushirikiano mkubwa zaidi wa kiusalama na Marekani.

India na Urusi zina ushirikiano wa karibu wa kutoka enzi za Vita Baridi, na Urusi ndiye muuzaji wake mkuu wa silaha.