1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Mawaziri wa Israel na Palestina kuhudhuria mkutano wa EU

22 Januari 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa Israel na mamlaka ya Palestina wanatarajiwa kukutana na wenzao wa Umoja wa Ulaya katika wakati ambapo Umoja huo unazingatia kuchukua hatua kuelekea kupatikana kwa amani.

https://p.dw.com/p/4bWVP
Waziri wa mambo ya nje wa mamlaka ya Palestina Riyad al-Maliki
Waziri wa mambo ya nje wa mamlaka ya Palestina Riyad al-MalikiPicha: Shannon Stapleton/REUTERS

Israel Katz na Riyad al-Maliki watashiriki katika nyakati tofauti mkutano na mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia, Misri na Jordan pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu pia watashiriki mkutano huo.

Kuelekea mkutano huo, Umoja wa Ulaya umetuma nyaraka ya majadiliano kwa nchi wanachama 27 ikipendekeza hatua za kuchukuliwa ili kufikia amani katika mzozo wa Israel na Hamas.