Marekani yataka msaada wa silaha kwa Sudan usitishwe
30 Aprili 2024Balozi wa Marekani Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kuongeza kwamba El Fasher mji mkuu pekee katika jimbo la Darfur ambao haujashikiliwa na vikosi vya kijeshi uko "kwenye ukingo wa mauaji makubwa."
Thomas-Greenfield ameongeza kwamba kuna ripoti za kuaminika kwamba vikosi vya RSF pamoja na washirika wake wameteketeza vijiji kadhaa magharibi mwa El Fasher na kuna mpango wa mashambulizi karibu na mji huo.
Soma zaidi: Nani anawaunga mkono makamanda wanaoipigania mamalaka Sudan?
Sudan ilitumbukia katika mzozo mnamo Aprili 2023 kufuatia mvutano baina ya majenerali wawili, Abdel Fattah Burhan anayeongoza vikosi vya serikali na Mohammed Hamdan Dagalo anayeongoza wanamgambo wa RSF.
Mzozo huo umesababisha maelfu ya watu kuuwawa na wengine mamilioni kukimbia makaazi yao.