Marekani yaahidi dola bilioni 2 za msaada kwa mipango ya UN
30 Desemba 2025
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema mkataba wa maelewano unaoelezea mtazamo mpya wa ufadhili ulitiwa saini Geneva hapo jana.
Hayo ni wakati utawala wa Rais Donald Trump ukipunguza misaada ya kigeni ya Marekani na kuyaonya mashirika ya Umoja wa Mataifa kwamba yanapaswa "kubadilika au kuangamia katika wakati ambao kunashuhudiwa changamoto mpya za kifedha.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, amesema makubaliano hayo yanabadilisha kwa kiasi kikubwa jinsi mipango ya Marekani inafadhili na kusimamia shughuli za kibinadamu za Umoja wa Mataifa, kuhakikisha kwamba maisha zaidi yanaokolewa kwa kutumia kiasi kidogo cha ufadhili.
Kwa upande wake, mratibu wa Misaada ya Dharura ya Umoja wa Mataifa Tom Fletcher aliishukuru Marekani kwa kujitolea kwake kwa shuguli za kibinadamu.